IQNA

Shughuli za Qur'ani za Waislamu Mashia Ulimwenguni Zaarifishwa

21:20 - August 11, 2021
Habari ID: 3474180
TEHRAN (IQNA) - Shughuli za juu za Qur'ani za Waislamu wa madhehebu ya Shia katika sehemu tofauti za ulimwengu zimearifishwa katika sherehe ya kufunga toleo la kwanza la "Tuzo ya Ulimwengu 114".

Hafla hiyo ilifanyika mnamo Agosti 9 katika ukumbi wa mikutano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahl-ul-Bayt (AS) katika mji mtakatifu wa Qom.

Hafla hiyo ilirushwa mubashara kwa njia ya intaneti kwa lugha za Kifarsi, Kiarabu na Kiingereza.

Kikao hicho kilichoandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Ahl-ul-Bayt (AS), kilifanyika kwa lengo la kutambua na kuthamini shughuli za Qur'ani na kuunda mtandao wa mipango ya Qur'ani ya wafuasi wa Ahl-ul-Byat (AS).

Tofauti ambayo tuzo hiyo ilikuwa nayo na hafla zingine na mashindano hayo ni kwamba hakuna mtu aliyealikwa kushiriki shindano hilo lakini waandaaji walitambua shughuli za Qur'ani na kuchagua na kutambulisha bora zaidi.

Katika duru ya kwanza ya tuzo, lengo lilikuwa kwenye shughuli za sanaa, vyombo vya habari na utengenezaji wa aplikesheni za kompyuta na simu za mkononi.

3989164

captcha