IQNA

Maonyesho ya ‘Uhusiano wa Kiutamaduni wa China na Ulimwengu wa Kiislamu’

22:03 - September 12, 2021
Habari ID: 3474288
TEHRAN (IQNA)- Jumba la Makumbusho la Louvre Abu Dhabi nchini UAE limetangaza kuandaa maonyesho ya ‘Uhusiano wa Kiutamaduni wa China na Ulimwengu wa Kiislamu’ ambayo yataanza Oktoba 6 2021 na kuendelea hadi Februari 12 2022.

Maonyesho hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Jumba la Makumbusho la Louvre Abu Dhabu kwa ushirikiano na Jumba la Kitaifa la Makumbusho Guimet la Ufaransa kwa himaya ya Jumba la Makumbusho la Ufaransa. Maoneysho hayo yataonyesha maingiliano ya kiutamaduni na kisanaa baina ya staarabu za China na ulimwengu wa Kiislamu kuanzia karne za 8 hadi 18 Miladia.

Maoneysho hayo yatawasilisha taswira za maingiliano ya staarabu hizo mbili kuanzia Bara Arabu, Asia ya Kati, Bahari ya Hindi hadi China na Vietnam ambapo yatadhihirihsa taswira ya uhusiano mrefu na tajiri.

3475678

Kishikizo: china ، louvre ، kiislamu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha