IQNA

'Msahafu Mkubwa Zaidi' duniani katika maonyesho ya Expo 2020 Dubai

12:25 - August 31, 2021
Habari ID: 3474242
TEHRAN (IQNA)- Msahafu ambao umetajwa kuwa mkubwa zaidi duniani utaonyeshwa katika maonyesho ya Expo 2020 Dubai ambaye yanatazamiwa kuanza mjini humo baadaye mwezi Oktoba.

Kwa mujibu wa taarifa Msahafu huo wa aina yake umeandikwa kwenye turubai na maandishi yameandikwa kwa aluminiumu na dhahabu. Aidha inaaminika kuwa ni msahafu wa aina yake katika historia ya Uislamu.

Kazi hii ni ya Mpakistani ambaye ameamua kuweka historia kwa kuandika aya za Qur'ani Tukufu kwa njia maalumu kwa mara ya kwanza. Shahid Rassam alianzisha mradi wake huo miaka mitano iliyopita na amepata zawadi kadhaa za kimataifa kutokana na mradi wake huo na hivyo anatazamia kuonyesha kazi yake hiyo katika maonyesho hayo ya kimataifa ya Dubai yatakayoanza Oktoba 20 na kuendelea kwa miezi sita.

Msahafu huo una urefu wa futi 8.5 na upana wa futi 6.5 na una jumla ya kurasa 550.

3475591

captcha