IQNA

13:31 - September 22, 2021
News ID: 3474327
TEHRAN (IQNA)- Ufalme wa Saudi Arabia umeandaa uchunguzi wa maoni kuhusu kupiga marufuku somo la Qur’ani katika vyuo vikuu vya nchi hiyo jambo ambalo limeibua mijadala mikali katika mitando ya kijamii.

Kwa mujibu wa taarifa utawala wa Saudia umeandaa uchunguzi huo wa maoni kupitia ukurasa wake wa Twitter uliopewa jina la @p_referendum  ambapo wananchi wameulizwa watoe maoni yao kuhusu pendekezo la kufuta somo la Qur’ani ambalo kwa sasa ni lazima kwa wanafunzo wanaosoma taaluma zote nchini humo.

Pendekezo hilo lina wengi wanaolipinga na pia kuna wengine ambao wameliunga mkono.

Wizara ya Elimu ya Saudia ina muundo mpya wenye lengo la kuteta mabadiliko katika mfumo wa elimu nchini humo na moja ya sera zinazofuatwa ni kama hiyo ya kufuta somo la Qur’ani  ambalo limekuwa lazima kwa wale wanafunzo wote wa vyuo vikuu.

Katika miaka ya hivi karibuni utawala wa Saudia katika kipindi cha Mfalme Salman umetekeleza mabadiliko mengi ambayo yanapingwa na wasomi wa kidini nchini humo.

3999317

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: