IQNA

Washiriki wa Mashindano ya Kitaifa ya Qur’ani Iran waongezeka mara tatu

13:54 - September 30, 2021
Habari ID: 3474362
TEHRAN (IQNA)- Idadi ya washiriki wa Mashindano ya Kitaifa ya Qur’ani ya Iran mwaka huu imeongezeka mara tatu ikilinganishwa na mwaka jana.

Hayo yamedokezwa na mkuu wa masuala ya Qur’ani katika Shirika la Wakfu la Iran Medhi Qarasheihklu ambaye amesema jumla ya watu 31,000 walishiriki katika mashindano hayo katika ngazi za mikoa na kitaifa.

Qarasheikhlu ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika sherehe za kukamilika mashindano ya Qur’ani katika mkoa wa Gorgan kaskazini mashariki mwa Iran.

Amesema katika Shirika la Wakfu la Iran limekuwa likiandaa mashindano ya Qur’ani kitaifa kwa zaidi ya miaka 40 sasa na kuongeza kuwa mashindani ya kitaifa yatafanyika baina ya Desemba 2021 na Januari 2022 na washindi watawakilisha Iran katika mashindano ya kimataifa.

4001344

captcha