IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Washindi wa Mashindano ya 47 ya Kitaifa ya Qur'ani ya Iran Watunukiwa

22:56 - December 19, 2024
Habari ID: 3479921
IQNA - Baada ya shughuli za miezi kadhaa, Mashindano ya 47 ya Kitaifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yalifikia tamati katika hafla ya Alhamisi asubuhi.

Washindi wa kategoria tofauti katika kitengo cha wanaume walitangazwa na kutunukiwa katika hafla hiyo, iliyofanyika katika Ukumbi Mkuu wa Sala (Musalla) wa Tabriz kaskazini magharibi mwa Iran kwa ushiriki wa maafisa kadhaa wa Qur'ani, kidini na kisiasa.

Jopo la majaji lilimtaja Mohammad Mehdi Rezaei kutoka Isfahan kuwa mshiriki bora zaidi katika kuhifadhi Qur’ani nzima.

Katika qiraa au usomaji wa Qur’ani, Seyed Jassem Mousavi kutoka Isfahan alinyakua tuzo ya juu huku katika mashindano ya Tarteel, Mehdi Foroughi kutoka Qom alichukua nafasi wa kwanza.

Seyed Mehdi Banihashemi kutoka Isfahan, Amir Hadi Bairami kutoka Ardebil na Mohammad Hossein Kohan Mehrabad kutoka Khorasan Razavi walikuwa washindi wa juu katika kuhifadhi Juzuu 20 za Quran, kuhifadhi Qur'ani nzima kwa ajili ya vijana chini ya miaka 18 na usomaji wa Qur'ani kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 18 mtawalia.

Mashindano hayo ni moja ya matukio ya fahari ya Qur'ani nchini Iran.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Shirika la Masuala ya Wakfu na Misaada ya Iran yanalenga kukuza utamaduni wa Qur'ani na kubainisha nafasi ya mafundisho ya Mwenyezi Mungu katika jamii. Washindi wakuu wa shindano hilo wataiwakilisha Iran katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kote duniani.

4255021

Habari zinazohusiana
captcha