Kwa mujibu wa taarifa kamati maalumu imeundwa kuwachagua waalimu bora zaidi wa taaluma ya kuhifadhi Qur'ani nchini Iran.
Wawakilishi wa Wizara ya Utamaduni na Muongozi wa Kiislamu, Kanali ya Qur'ani ya IRIB, Taasisi ya Darul Qur'an Karim na taasisi zingine kadhaa wanaunda kamati hiyo ambayo itakuwa na matawi katika miko yote ya Iran.
Imedokezwa kuwa kati ya vigezo vya kuchaguliwa waalimu hao ni kwa kwa uchaguze wawe wamehifadhi Juzuu 10 za Qur'ani na wawe na uzoefu wa miaka mitano katika ufundishaji kuhifadhi Qur'ani Tukufu.
Mashindano ya 38 ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani ya Iran yanatazamiwa kufanyika Machi 2022 mjini Tehran.