IQNA

Kiongozi Muadhamu kwa mnasaba wa kuanza Wiki ya Basiji

Masuala yote ya nchi yanaweza kutatuliwa kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu

0:09 - November 25, 2021
Habari ID: 3474596
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe wa maandishi kwa mnasaba wa Wiki ya Jeshi la Kujitolea la Basiji na kusema kuwa: Mabasiji mnapaswa kuwa watatuzi wa masuala yote ya nchi na ya taifa kwa kumtegemea na kutawakali kwa Mwenyezi Mungu, Mjuzi na Muweza wa kila siku.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameyasema hayo Jumatano wakati akitoa mkono wa baraka kwa mnasaba wa kuanza Wiki ya Basiji humu nchini na kusisitiza kuwa, jeshi hilo la kujitolea la wananchi kama ilivyokuwa kwa vizazi vya kabla ya cha hivi sasa, wote ni wana wapendwa wa Imam Khomeini MA. 

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, mabasiji wanapaswa kudiriki vilivyo nafasi yao muhimu kama ambavyo wanapaswa pia kuelewa kwamba, kwa hima ya hali ya juu na kujiweka chini ya kivuli ya kutumia vizuri akili na fikra sahihi na kwa kutawakali na kumtegemea Mwenyezi Mungu Mjuzi na Muweza wa kila kitu, wanaweza kutatua masuala yote ya nchi na taifa na huo ni uzoefu mzuri lilio nao taifa la Iran kwa miongo kadhaa sasa.

Imam Khomeini MA, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliunda Jeshi la Kujitolea la Wananchi yaani Jeshi la Basiji, tarehe 26 Novemba 1979.

Katika kipindi cha miongo minne iliyopita, jeshi hilo limefanya kazi kubwa humu nchini katika nyuga tofauti za kiulinzi na kijeshi, kielimu na teknolojia na kwenye kila sekta liliyoingia.

Mafanikio yaliyopatikana nchini Iran kutokana na fikra hiyo ya kuwa na jeshi la Basiji ambalo ni nguzo muhimu sana ya Mapinduzi na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, imekuwa kigezo kizuri kinachofuatwa hivi sasa na mataifa mengine ya eneo hili.

4015887

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha