IQNA

19:28 - December 02, 2021
Habari ID: 3474628
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Wakfu ya Misri imeandaa mkutano wa kuchunguza hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa kwa ajili ya kuandaa Duruy a 28 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani.

Waziri wa Wakfu wa Miri Sheikh Mohammad Mukhtar Gomaa amehudhuria kikao hicho kilichojadili uandalizi wa mashindano hayo ambayo yamepengwa kufanyika Disemba 11 hadi 15 mjini Cairo.

Taarifa iliyotolewa baada ya kikao hicho imebaini kuwa mashindano yam waka huu yatakuwa na washiriki 74 na majaji 12 kutoka nchi mbali mbali duniani.

Gomaa amesema Pauni milioni mopja za Misri zimetengwa kwa ajili ya  washindi wa mashindano hayo  ya Qur'ani.

Kategoria za mashindano hayo zitakuwa ni pamoja na kuhifadhi Qur'ani TUkufu kikamilifu, Tajweed, Tartifl na ufahamu wa Qur'ani kwa wale ambao lugha yao asili ni Kiarabu.

Kategoria nyingine ya mashindano hayo itakuwa ni kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu kwa wale wasiozungumza luhga ya Kiarabu. Halikadhalika kutakuwa na kitengo cha kuhifadhi Qur'ani kwa walemavu. Mwaka huu pia kutakuwa na mashindano ya kufhidahi Qur;ani kwa watoto wenye umri wa miaka 12 na halikadhalika mashindano maalumu ya wanawake ya kuhifadhi Qur'ani.

3476761

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: