IQNA

Rais wa Misri ataka tafsiri ijumuishwe katika mashindano ya Qur’ani

18:59 - December 15, 2021
Habari ID: 3474676
TEHRAN (IQNA)- Rais Abdul Fattah el-Sisi wa Misri ametaka kipaumbele maalumu kipewe kwa tafsiri na ufahamu wa Qur’ani katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani nchini humo.

Rais el Sisi ameyasema hayo alipokutana na Waziri wa Wakfu Sheikh Mohammad Mukhtar Gomaa ambaye amemkabidhi ripoti ya mashindano ya kimataifa ya Qur’ani yaliyomalizika Cairo.

Katika kikao hicho, Rais el-Sisi amesema mashindano ya Qur’ani sasa hayapaswi kuzingatia tuu uwezo wa kuhifadhi Qur’ani tu bali kunapaswa kuwepo pia kategeroa kama vile Tafsiri na ufahamu wa Qur’ani.

Aidha amesisitiza kuhusu kuimarisha vipawa vya vijana na mabarobaro ambao wana vipaji katika Qur’ani Tukufu.

Kwa upande wake, Sheikh Gomaa amesema mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Misri yamehudhuriwa na washiriki wan chi mbali mbali duniani.

Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Misri yamefanyika Cairo kuanzia 11-15 Disemba 2021.

Mashindano hayo yalikuwa na washiriki 74 ambao wameshindana katika kategoria ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu.

4020861

captcha