IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran

Takwa la Iran katika mazungumzo ya Vienna ni kuondolewa vikwazo vya kidhalimu

19:09 - December 03, 2021
Habari ID: 3474632
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Muda wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesisitiza kuwa, taifa la Iran halitokubaliana na chochote katika mazungumzo yanayoendelea mjini Vienna Austria ghairi ya kuondolewa vikwazo vyote vya kidhalimu lilivyowekewa taifa hili la Kiislamu na madola ya kibeberu.

Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema hayo katika khutba za Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran  na kuongeza kuwa, ujumbe wa Iran katika mazungumzo hayo unawakilisha taifa shujaa ambalo limesimama imara kupigania malengo yake matukufu hadi tone lake la mwisho la damu na ambalo haliwezi kukubaliana na chochote ghairi ya kuondolewa vikwazo vyote vya kidhalimu vilivyowekwa na madola ya kibeberu.

Ameongeza kuwa, ujumbe wa Iran unaoshiriki kwenye mazungumzo ya Vienna unaundwa na watu wenye uzoefu na kwamba ujumbe huo unatangaza waziwazi msimamo wake kama ambavyo misimamo ya kuipinga Marekani inaonekana katika maneno na vitendo ya wajumbe hao wa Iran.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran vile vile ameipongeza Serikali ya 13 ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kusimamia na kuendesha vizuri zoezi la upigaji chanjo za ugonjwa wa UVIKO-19 baada ya kuingiza nchini kiwango cha kutosha cha chanjo hizo.

Ayatullah Khatami vile vile amekumbushia kuwadia tarehe 3 Disemba inayosadifiana na kumbukumbu ya mwaka aliouawa shahidi Sayyid Hassan Modarris na amesema: Shahid Modarris alikuwa miongoni mwa shakhsia wakubwa kiasi kwamba hata Imam Khomeini MA alikuwa akimuangalia kwa jicho hilo na mara nyingi alikuwa akimuenzi na kumtaja kwa wema mwanachuoni huyo.

4018044

captcha