IQNA

Hatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Hali ya dunia ya sasa inayokwenda kwa maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu

17:32 - December 10, 2021
Habari ID: 3474659
TEHRAN (IQNA)- Hatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa Iran ya leo ndiyo nchi yenye nguvu zaidi katika eneo la Magharibi mwa Asia, na iko katika nafasi ambayo hakuna nchi inayothubutu kuishambulia.

Hujjatul Islam Walmuslimin Kazem Seddiqi ameashiria mazungumzo ya nyuklia yanayoendelea uko Vienna na kusema: Serikali ya kimapinduzi na ya wananchi ina hamu ya kuwa na uhusiano mwema na nchi zote duniani na kuamiliana nazo kwa hikima na heshima. 

Ameongeza kuwa: "Anga hii mpya ambapo mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na mti huu adhimu umekita mizizi na kuimarika na kuweza kustahimili changamoto zote na mawimbi ya kimataifa ni kutokana na hali ya dunia ya sasa inayokwenda kwa maslahi yetu."

Amesema: "Marekani ilitekeleza njama zake katika pande tatu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu katika vipindi tofauti hususan katika zama za Donald Trump. Moja njama hizo ilifanywa na Wizara ya Fedha ya Marekani na ya pili Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi ambayo ililfanya safari katika nchi mbalimbali na kuzilazimisha nchi tofauti zisishirikiane na Iran. Hatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema njama nyingine zinafanywa na shirika la ujasusi la Marekani CIA ambalo limekuwa likifanya mikakati ya kuwachochea wananchi wa Iran dhidi ya utawala wa Kiislamu kupitia mashinikizo ya kiuchumi na vikwazo vya kimataifa tangu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini. 

Hujjatul Islam Walmuslimin Seddiqi amesema: “Hata hivyo kwa busara ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi na utambuzi, uvumilivu na utulivu wa wananchi, uhusiano huu usiotenganishwa kati ya wananchi na utawala wa Kiislamu, umewafanya Wamarekani wakiri kwamba hawakufanikiwa na kamwe hawataweza kufikia malengo yao." 

4019829

captcha