IQNA

Msikiti Canada watumika kama makazi kwa wasio na makao msimu wa baridi kali

13:08 - January 01, 2022
Habari ID: 3474751
TEHRAN (IQNA)- Msikiti wa Al Rashid huko Edmonton nchini Canada sasa unatumika kama makazi ya usiku kwa watu masikini wasio na nyumba katika kipindi hiki cha msimu wa baridi kali.

Wakuu wa Msikiti huo wamesema wataendelea kuwapa makazi watu masikini katika mwezi wa Januari wakati wa msimu wa baridi kali. Huduma hiyo imekuwa ikitolewa mwezi uliopita wa Disemba na sasa muhula wake umeongezwa kutokana na hali ya hewa ya baridi kali kuendelea.

Jumuiya ya Afya ya Akili Canada (CMHA) inasema katika mji wa Edmonton, kati ya Disemba 23 na 29 ilipokea simu 820 na Disemba 27 ilipokea simu 163 za misaada ya eneo la kulala kutokana na baridi kali iliyofika kiwango cha -33.  Aidha Disemba 28 wakati  kiwango cha baridi kali kilifika 135 watu 148 walipiga simu wakiomba msaada.

Hali hiyo ya baridi kali mjini Edmonton inatarajiwa kuendela kwa muda wa wiki mbili hivi na hivyo msikiti wa Al Rashid umeamua kuwasaidia wale wanaohitaji msaada.

Kwa muda wa miaka mitatu sasa Msikiti wa Al Rashid umekuwa ukitoa msaada kwa watu takribani 300 kila siku wakati wa msimu wa baridi.

3477177

captcha