IQNA

Mashindano ya Qur’ani ya Polisi Iran kufanyika mjini Mashhad

22:40 - January 09, 2022
Habari ID: 3474785
TEHRAN (IQNA)- Duru ya mwisho ya Mashindano ya 26 ya Kitaifa ya Qur’ani Tukufu ya Jeshi la Polisi Iran yatafanyika katika mji wa Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran.

Kwa mujibu wa mmoja kati ya maafisa wanaoandaa mashindano hayo, Jenerali Mohammad Bahrami, mashindano hayo yataanza Januari 23 hadi 25 katika Haram Takatifu ya Imam Ridha AS.

Washiriki katashindano katika qiraa, tartil na kuhifadhi Qur’ani Tukufu na halikadhalika adhana.

Maafisa 22,000 wa polisi kote Iran walishiriki katika mchujo wa kwanza na wa pili wa mashindano hayo katika miezi ya Novemba na Disemba. Bahrami amesema idadi ya washiriki mwaka huu imeongezeka kwa asilimia kumi ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Washindi katika mashindano hayo watawakilisha jeshi la polisi katika Mashindano ya Kitaifa ya Qur’ani ya Majeshi ya Iran yatakayofanyika Februari mjini Tehran.

4027272

captcha