IQNA

Spika mpya wa bunge ateuliwa Iraq, waziri mkuu ampongeza

16:56 - January 10, 2022
Habari ID: 3474788
TEHRAN (IQNA)- Waziri Mkuu wa Iraq ametoa mkono wa pongezi kufuatia kuchaguliwa kwa mara ya pili Mohammed al Halbousi kuwa Spika mpya wa Bunge la Iraq katika duru ya pili ya utendaji wa bunge hilo.

Musfata al Kadhimi amendika katika ujumbe aliotuma kwamba: "Leo ni siku kubwa  na njema katika historia ya Iraq kwa ajili ya kuimarisha umoja na mshikamano wa wananchi katika njia ya kutekeleza marekebisho na kudumisha umoja nchini." 

Al Kadhimi amempongeza al Halbousi na naibu wake kwa kuchaguliwa tena bungeni. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Mohammed al Halbousi amemkaribisha Waziri Mkuu Mustafa al Kadhii katika ofisi yake huko Baghdad baada ya kuchaguliwa Spika mpya kwa ajili ya duru ya nne ya Bunge la Iraq. 

Kikao cha kwanza cha Bunge jipya la Iraq kilifanyika jana Jumapili kwa kuwakutanisha wabunge; na Mohammed al Halbousi alichaguliwa kuwa Spika wa mpya wa duru ya nne ya bunge hilo kwa kupigiwa kura 200 za ndio na wabunge. 

Al Halbousi ni mbunge wa Bunge la Iraq tangu mwaka 2014; na amekuwa spika wa bunge hilo kuanzia mwaka 2018. 

4027495

captcha