IQNA

Wanawake Waislamu katika Gadi ya Pwani Ufilipino waruhusiwa kuvaa Hijabu

17:00 - February 04, 2022
Habari ID: 3474888
TEHRAN (IQNA)- Wanawake Waislamu wanaohudumu katika Kikosi cha Gadi ya Pwani ya Ufilipino sasa wanaruhusiwa kuvaa Hijabu ikiwa ni katika jitihada za kuwahimiza wanawake Waislamu wajiunge na kikosi hicho.

Gadi ya Pwani ya Ufilipino (PCG) imetangaza kuwa hivi sasa ina maafisa 1850 Waislamu na miongoni mwao kuna wanawake 200.

"Gadi ya Pwani ya Ufilipino imeidhinisha Hijabu kama sare rasmi ya maafisa wanawake Waislamu," taarifa ya gadi iyo imesema na kuongeza kuwa sera hiyo imeshaanza kutekelezwa.

Aidha taarifa hiyo imesema Waislamu wamepongeza hatua hiyo ya kujumuisha Hijabu kama sare kwani itapelekea wanawake wengi Waislamu wapate motisha wa kujiunga na kikosi hichyo.

Pendekezo la kujumuisha mtandio wa Kiislamu kama sare lilitolewa mwaka jana na imamu katika gadi hiyo Sheikh Kapteni Alicman Borowa aliyesema hatua hiyo ingepelekea wanawake Waislamu wahisi hawajatengwa.

Gadi ya Pwani ya Ufilipino imeiga uamuzi wa kuruhusu Hijabu katika Jeshi la Ufilipino, Kikosi cha Polisi Ufilipino na pia idara ya magereza nchini humo.

Ufilipino ni nchi iliyo kwenye eneo la Funguvisiwa la Malay huko kusini-mashariki mwa Asia. Ufilipino ina visiwa 7,641 vinavyohesabiwa katika makundi matatu yanayoitwa kufuatana na ujirani na visiwa vikubwa vya Luzon, Visaya, Mindanao.

Kwa mujibu wa takwimu, idadi ya Waislamu Ufilipino ni zaidi ya milioni 5.1, yaani asilimia 6 ya watu wote wa nchi hiyo. Zaidi ya nusu ya Waislamu wanaishi katika kisiwa cha kusini cha Mindanao.

captcha