IQNA

Shule za Qur'ani Algeria zafungwa siku 10 kutokana na ongezeko la COVID-19

16:44 - January 22, 2022
Habari ID: 3474835
TEHRAN (IQNA) – Shule za Qur'ani zimefungwa kwa muda wa siku 10 kufuatia ongezeko kubwa la maambukizi ya COVID-19.

Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini Algeria imetangaza kuwa shule zote za Qur'ani nchini humo zitafungwa kwa siku 10.

Hatua hiyo imekuja baada ya vituo vingine vyote vya elimu navyo kufungwa katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika ili kukabiliana na wimbi jipya la COVID-19.

Shule zote Algeria zilifungwa Alhamisi kwa muda wa siku 10 huku ikitarajiwa kuwa hatua hiyo itaweza kupunguza maambukizi ya aina mpya ya COVID-19 ijulikanayo kama omicron.

"Hali ni ya kushutua na ongezeko la maambukizi linazidisha mashinikizo kwa vituo vya afya, mahospitali na vyumba vya wagonjwa mahututi," amesema daktari mwandamizi Nabil Melian.

4030200

captcha