IQNA

Harakati za Qur'ani

Zaidi ya Waalgeria Milioni 1.2 wanajifunza Qur’ani Tukufu katika vituo maalumu

21:16 - June 21, 2024
Habari ID: 3478995
IQNA - Waziri wa Wakfu wa Algeria amesema idadi kubwa ya wanafunzi wanajifunza Qur'ani katika vituo vya Qur'ani kote katika nchi hiyo kaskazini mwa Afrika.

Akizungumza katika hafla iliyofanyika kuzindua shule ya Qur'ani katika mji mkuu wa Algiers, Youcef Belmehdi amepongeza kushamiri kwa shule za Qur'ani na vituo vya Qur'ani nchini humo, Kituo cha Habari cha Algeria kimeripoti.

Amesema zaidi ya Waalgeria milioni 1.2 wanasoma kozi za Qur'ani katika shule na vituo vya Qur'ani.

Wanajifunza kuhifadhi Qur'ani, usomaji na tafsiri, alibainisha.

Waziri wa Wakfu alishukuru juhudi za wale wanaosimamia shule za Qur'ani za majira ya kiangazi na kusema wakati wanafunzi wapatao 500,000 wamejiandikisha kujifunza Qur'ani katika shule hizo mwaka jana.

Belmehdi amesema wizara hiyo pia imeandaa shughuli nyingine za Qur'ani msimu huu wa kiangazi, zikiwemo kambi za Qur'ani za majira ya kiangazi.

Ameongeza kuwa, lengo kuu la shughuli hizo ni kuinua kizazi kwa misingi ya mafundisho ya Kitabu Kitakatifu.

Algeria ni nchi ya Kiarabu iliyoko Afrika Kaskazini. Waislamu ni takriban asilimia tisini na tisa ya wakazi wa nchi hiyo.

4222321

Habari zinazohusiana
Kishikizo: algeria qurani tukufu
captcha