IQNA

22:51 - July 27, 2021
News ID: 3474133
TEHRAN (IQNA)- Mamlaka ya Algeria iliamuru kufungwa kwa misikiti katika maeneo mengi ya nchi kutokana na ongezeko la maambukizi ya COVID-19, haswa aina mpya ya Delta.

Wizara ya Awqaf na Maswala ya Kidini ya Algeria ilitangaza kuwa misikiti katika majimbo 35, pamoja na mji mkuu Algiers, itafungwa.

Wizara hiyo ilisema kozi za Qur'ani na mihadhara ya kidini pia itasitishwa na vituo vyote vya Kiislamu na kitamaduni vitafungwa pia. Aidha wizara hiyo imesisitiza haja kuzingatia kanuni za kiafya ili kuzuia kuenea COVID-19.

Vizuizi vingine pia vimewekwa tena kwenye mikusanyiko kutoka Jumatatu ili kukabiliana na kuenea haraka kwa aina mpya COVID-19 inayoambukiza zaidi ya Delta ambayo imesababisha kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa.

Hatua hizo, ambazo zitatumika kwa majimbo 35 kati ya 58, ni pamoja na kufunga vituo vya kitamaduni, kumbi za starehe, fukwe na masoko ya gari yaliyotumiwa, na pia amri ya kutotoka nje ya saa mbili usiku hadi 12 asubuhi, ilisema taarifa kutoka ofisi ya waziri mkuu.

Mikusanyiko yote, pamoja na sherehe za harusi zitapigwa marufuku, wakati migahawa itaruhusiwa kutoa huduma za kuchukua tu.

Nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika hadi sasa imeripoti jumla ya maambukizi 163,660, ikiwa ni pamoja na vifo 4,087, tangu janga hilo lilipoanza mapema mwaka jana.

3986705

Tags: algeria ، waislamu ، covid 19 ، delta
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: