IQNA

Shule London yazuia Sala ya Ijumaa ya wanafunzi Waislamu

19:53 - January 26, 2022
Habari ID: 3474857
TEHRAN (IQNA)- Wanafuzni Waislamu katika Shule ya Upili ya Park High mtaa wa Stanmore nchini London wanasema mwalimu mmoja shuleni hapo amewanyima idhini ya kusali Sala ya Ijumaa katika uwanja wa shule.

Shule hiyo katika mji mkuu wa Uingereza sasa inakabliwa na mashinikizo kutokana na hatua hiyo ya kuwanyima wanafunzi Waislamu haki ya kusali Sala ya Ijumaa.

Wanafunzi hao Waislamu wanasema walilazimika kusali nje baada ya shule kuwanyima idhini ya ksali ndani ya moja ya vyumba vya darasa.

Shule ya Park High imetoa taarifa na kukanusha kuwa imewazuia wanafunzi kusali Sala ya Ijumaa lakini haikutoa maelezo kuhusu sababu ambayo ilipelekea wasali katika uwanja wa shule hiyo.

Imedokezwa kuwa tatizo kama hilo liko katika shule nyingi nchini Uingereza ambapo wanafunzi Waislamu wanabaguliwa na kunyimwa idhini ya kusali Sala ya Ijumaa.

3477550/

Kishikizo: waislamu uingereza
captcha