IQNA

Waziri Mkuu wa Pakistan ataka hatua za kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu

18:09 - February 25, 2022
Habari ID: 3474974
TEHRAN (IQNA)- Waziri Mkuu wa Pakistan mran Khan anasema ni muhimu kufanya kazi katika kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu kote ulimwenguni.

Alisema hayo katika ziara yake ya kutembelea Msikiti Mkuu wa Moscow ambapo Mufti Mkuu Sheikh Ravil Gaynutdin alimpokea Waziri Mkuu.

Imran Khan pia alisisitiza haja ya kuunda maelewano ya dini mbalimbali kwa ajili ya kuishi pamoja kwa amani katika ulimwengu unaozidi kugawanyika. Kuhusiana na hili, Waziri Mkuu amepongeza uelewa wa Rais Vladimir Putin wa Russia kuhusu hisia ambazo Waislamu walizonazke kwa Mtukufu Mtume Muhammad SAW.

Hapo awali, katika mkutano wake na Mkuu wa Jamhuri ya Chechnya Ramzan Kadyrov, Waziri Mkuu Imran Khane amepongeza ujenzi mpya wa Grozny na upanuzi wa haraka wa Chechenya chini ya uongozi wa Ramzan Kadyrov.

Alisema uhusiano kati ya Pakistan na Urusi uko kwenye mwelekeo mzuri  na  alihimiza kukuza ushirikiano kati ya majimbo tofauti ya Pakistani na maeneo mbali mbali Russia.

3477953

captcha