Katika sherehe iliyofanyika Sharajah wiki hii, Akademia ya Qur’ani UAE ilitangaza kupanua shughuli zake katika nchi zote za Amerika Kaskazini.
Katibu mkuu wa akademia hiyo, Sheikh Sherzad Abdul Rahman Taher na wanazuoni kadhaa walihudhuria sherehe hiyo.
Akizungumza katika kikao hicho, Sheikh Sherzad alisema akademia hiyo imepiga hatua kubwa katika muda mfupi tokea ianzishwe na kwamba imeanzisha taasisi za kitaalamu za kuhudumia Qur’ani Tukufu katika nchi 155 kote duniani.
Naye Aisha Al Ansari, mkuu wa Kitengo cha Kimataifa cha Akademia ya Qur’ani UAE amebainisha furaha yake kutokana na kuanzishwa huduma za akademia hiyo katika nchi za Amerika Kusini
Halikadhalika amesema mwaka jana walfanikiwa kueneza shughuli zao katika nchi zote za Afrika na sasa jitihada zinafanyika kueneza shughuli zao kote barani Asia.
4044040