IQNA

Amnesty yaikosoa Ufaransa kwa kuwabagua Waislamu

23:02 - March 30, 2022
Habari ID: 3475088
TEHRAN (IQNA)- Katika ripoti yake ya kila mwaka kuhusu hali ya haki za binadamu duniani, shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International lilikosoa rekodi ya haki za Ufaransa, hususan sera yake kuhusu Waisamu na wakimbizi.

Ripoti hiyo inasema mapungufu ya haki za Ufaransa na 'viwango viwili' au undumakuwlili huwaacha wengi wakiishi katika hali duni na ya kufedhehesha huku Waukraine wanaokimbia oparesheni za kijeshi za Russia wakichukuliwa tofauti na wale kutoka nchi nyingine.

Nathalie Godard, mkurugenzi wa utekelezaji wa Amnesty International Ufaransa, akiwasilisha ripoti kwa vyombo vya habari Jumanne ametoa mfano na undumakuwili huo ambao amesema umedhihirika jinsi viongozi wa Ufaransa wanavyozungumza kuhusu wakimbizi Waukraine na jinsi walivyozungumza mwaka jana kuhusu Waafghanistan waliotoroka nchi ya baada ya Taliban kuingia madarakani.

Serikali ya Ufaransa imeweka mpango wa kuwakaribisha takriban raia 100,000 wa Ukraine wanaokimbia oparesheni za kijeshi za Russia nchini humo, wakati serikali hiyo hiyo ya Ufaransa imezungumza kuhusu kujikinga na mawimbi  ya wahamiaji kutoka maeneo mengine.

Hiki ni "kielelezo cha viwango viwili" linapokuja suala la wakimbizi, alisema Godard.

Huko Calais, ambapo wahamiaji wengi hukusanyika kujaribu kuvuka bahari na kuingia Uingereza, "kwa miaka mingi, wakimbizi wanaishi katika mazingira ya fedheha na ya kudhalilishwa," shirika hilo lilisema.

Amnesty pia ilisema Ufaransa ni miongoni mwa nchi 67 zilizopitisha sheria mwaka 2021 zinazozuia uhuru wa kujieleza na kujumuika.

Kundi la kutetea haki za binadamu "liliibua wasiwasi kuhusu ufuatiliaji wa watu wengi na haki za uhuru wa kujieleza na kujumuika" nchini Ufaransa, na mfano wa wazi ni sheria ya kupambana na ugaidi iliyopitishwa Julai 2021 ambayo inaruhusu udhibiti zaidi wa kiutawala na ufuatiliaji kwa washukiwa wa ugaidi.

Sheria inayoitwa "sharia ya kupambana na wanotaka kujitenga" iliyoanza kutumika mnamo Agosti 2021 ina hatari ya "kukuza fikra potofu" kuhusu Waislamu, kwa kuwahusisha na magaidi.

Licha ya Ufaransa kuwa na idadi kubwa ya Waislamu miongoni mwa nchi za Ulaya lakini imeweka vizuizi vingi dhidi ya uhuru wa kuabudu kwa Waislamu wa nchi hiyo.

4045591

captcha