IQNA

Liberia yaruhusu Hijabu shuleni kwa muda

15:39 - April 24, 2022
Habari ID: 3475161
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Liberia inayoongozwa na Rais George Weah imechukua hatua ya aina yake kuruhusu kuwaruhusu wanafunzi wa kike Waislamu wake kuvaa Hijabu wakiwa chuoni wakati wa kuadhimisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Hatua hiyo adimu, ambayo ni ya kwanza ya kihistoria kwa Liberia, imekuja baada ya miaka kadhaa ya jitihada za viongozi wa Kiislamu ambao pia wamelalamika kwamba Siku Kuu ya Idul Fitr haiheshimiwi kitaifa, ikilinganishwa na sikukuu za Wakristo.

Kwa miongo kadhaa, idara ya shule za  za umma katika Kaunti ya Montserrado inayojumuisha mji mkuu wa Liberia, Monrovia,  ambayo inajulkana kama the Monrovia Consolidated School System (MCSS) imeegemea kwenye sherehe za Kikristo, ukisimamisha shughuli za masomo wakati wa sherehe hizo.

Katika taarifa iliyotangaza hatua hiyo, wakuu wa elimu nchini Liberia wamesema kwamba sababu za msingi za uamuzi wa kuruhusu Hijabu shuleni kwa muda ni kuendeleza “ustahimilivu wa kidini, pamoja na umoja katika utofauti, na heshima kwa kila dini ya kila mtu.”

"Wanafunzi wote wa kike wa eneo la Monrovia ambao ni wa imani ya Kiislamu wanaruhusiwa kuvaa Hijabu katika mwezi huu mtukufu wa mfungo na shule za MCSS zitafungwa Jumatatu, Mei 2, 2022, kwa ajili ya kuadhimisha 'Eid al-Fitr' mwishoni mwa Ramadhani," MCSS ilisema katika taarifa yake Jumamoso. MCSS, pia imejiunga na serikali katika kuwapongeza wanafunzi na wafanyakazi wa imani ya Kiislamu wakati huu wa saumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani."

Hatua ya hivi punde ya utawala wa Weah inaakisi uamuzi kama huo ambao serikali yake ilichukua mwaka wa 2019 wakati, kwa mara ya kwanza katika historia ya Liberia, aliwapa likizo watumishi wa umma Waislamu kusherehekea Eid al-Fitr.

Rais Weah pia alifunga bao lingine la kihistoria alipomteua Usmane T. Jalloh kama mshauri rasmi wa kwanza wa dini ya Kiislamu nchini humo, kumshauri Rais kuhusu masuala yanayohusiana na jumuiya ya Kiislamu.

Mashirika ya Kiislamu tangu wakati huo yamekaribisha hatua hiyo. Hata hivyo, waliendelea kutoa wito wa kutambuliwa rasmi au kuadhimishwa kwa sikukuu kuu za kidini za Kiislamu na kutaja Sikukuu ya Krismasi na Pasaka, kama mifano ya likizo za Kikristo zinazotambulika rasmi.

/4049238

Kishikizo: liberia waislamu hijabu
captcha