Thamani ya Misahafu hiyo imetathminiwa kuwa ni zaidi ya dola za Marekani 350,000.
Mmiliki wa shule hiyo, Yaya Keita, alisema Misahafu hiyo itasamabzwa miongoni mwa Waislamu hasa wale ambao hawana uwezo wa kununua.
Keita alifichua kwamba Jumuiya ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu yenye makao yake makuu Amman, Jordan na Mohamed Sekou wa Taasisi ya Perere kwa Maendeleo ya Binadamu nchini Guinea yalifadhili usafirishaji wa kontena hilo hadi Liberia.
Alieleza kuwa taasisi yake itashirikiana na Baraza la Kitaifa la Waislamu wa Liberia kwa madhumuni ya kuhakikisha kuwa nakala za Quran zinawafikia Waislamu na taasisi za Kiislamu kote nchini.
Liberia ni nchi iliyoko kwenye pwani ya magharibi ya Afrika, ikipakana na Sierra Leone, Guinea, na Côte d'Ivoire.
Uislamu nchini Liberia unatekelezwa na takriban asilimia 12 ya watu wote.
3481186