IQNA

Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani Liberia

13:13 - June 20, 2016
Habari ID: 3470402
Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu yamefanyika hivi karibuni nchini Liberia katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo ambayo ni ya 17 yamefanyika katika mji mkuu Monrovia katika Msikiti wa Clara Town. Mashindano hayo yalikuwa na washiriki 46 ambao walishindana katika kategoria 11 ikiwa ni pamoja na kuhifadhi Qur'ani kikamilifu.

Jaji mkuu katika mashindano hayo, Imam Abdullah Mansaray wa Msikiti wa Clara Town amewashukuru Waislamu wa eneo hilo kwa ushirikiano wao katika kuandaa mashindano hayo. Aidha amewashukuru wanafunzi walioshiriki kwa umahiri na ustadi waliooneysha katika kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu.

Mashindano hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Umoja wa Dawah katika Ummah Liberia.

Imam Mansaray ametangaza kuwa matokeo ya mashindano hayo yaliyofanyika kati ya Juni 12 na 19 yatatangazwa tarehe 17 Julai.

Liberia ni nchi iliyo Afrika Magharibi na Waislamu wanakadiriwa kuwa asilimia takribani 15 kati ya wakaazi milioni nne nchini humo.

3460145

captcha