IQNA

Taarifa ya OIC kuhusu Msikiti wa Al Aqsa

19:29 - April 27, 2022
Habari ID: 3475174
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imesisitiza kuwa, mji mtakatifu wa Quds (Jerusalem) pamoja na Msikiti wa al Aqsa ni mstari mwekundu kwa Umma wa Kiislamu na amani na utulivu hauwezi kupatikana bila ya kukombolewa maeneo hayo matakatifu kutoka kwenye makucha ya utawala wa Kizayuni.

Katika mji wa Quds ndiko uliko Msikiti wa al Aqsa ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu. Ni eneo ambalo haliwezi kutenganishika na maeneo mengine ya Palestina, na ni moja ya maeneo matatu matukufu zaidi kwa Umma wa Kiislamu.

Msikiti wa al Aqsa ni nembo ya Uislamu katika mji wa huo wa Quds ambao pia unajulikana kama Baytul Muqaddas lakini mara kwa mara Wazayuni maghasibu wanafanya jinai, ukatili na njama za kila namna dhidi ya maeneo hayo matakatifu ya Waislamu.

Kituo cha upashaji habari cha Palestina kimeripoti kuwa, wanachama wa OIC walisema jana katika kikao chao cha mjini Jeddah kwamba kuna udharura wa kuunganishwa jitihada za wanachama wote wa jumuiya hiyo katika ukombozi wa Quds na matukufu ya Waislamu na kupambana kwa pamoja na jinai za utawala wa Kizayuni. Washiriki wa kikao hicho wametilia mkazo pia wajibu wa kuwaunga mkono wananchi wa Palestina mbele ya mashambulio ya kinyama wanayofanyiwa na Wazayuni.

Tamko hilo la mwisho la kikao hicho limesema pia kuwa, hujuma na uvamizi wa Wazayuni dhidi ya wananchi wa Palestina hasa kwenye mji wa Quds ni vitendo vilivyo kinyume cha sheria vinavyofanywa na utawala wa Kizayuni katika mji huo mtakatifu ni katika njama za kupotosha uhakika wa kihistoria kuhusu mji wa Baytul Muqaddas na Msikiti wa al Aqsa.

4052507

Kishikizo: oic aqsa quds tukufu
captcha