IQNA

Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu

Nchi za Kiislamu ziunge mkono Palestina katika mapambano na utawala wa Kizayuni

7:25 - April 29, 2022
Habari ID: 3475182
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu imetangaza kuwa njia ya kuuangamiza utawala wa Kizayuni ni kuimarisha safu ya Jihadi na mapambano mataifa sambamba na nchi za Kiislamu kutangaza uungaji mkono wao wa pande zote kwa wananchi waliodhulumika wa Palestina.

Taarifa hiyo ya Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu imetolewa kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds na kuongeza kuwa: Mapambano ya wananchi wa Palestina, kuimarishwa Jihadi na utamadunin wa kufa shahidi na pia misaada ya uungaji mkono wa mataifa na nchi za Waislamu kwa wananchi madhulumu wa Palestina ni mambo muhimu kwa ajili ya kuianisha mustakbali wa baadaye wa Palestina.  

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imeeleza kuwa, ni zaidi ya miongo saba sasa ambapo Umma wa Kiislamu unakabiliwa na kikwazo kinachojulikana kwa jina la utawala ghasibu wa Israel; utawala ambao unayakalia kwa mabavu maeneo ya ardhi za Kiislamu kwa msaada na himaya ya Marekani. Mwasisi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imamu Ruhullah Khomeini (M.A) aliyataja maeneo hayo yanayokaliwa kwa mabavu kuwa ni sehemu ya mwili wa Uislamu huku maelfu ya wake kwa waume wa Umma wa Kiislamu wakiuliwa na kukandamizwa katika ardhi hizo. 

Leo Ijumaa tarehe 29 Aprili yaani  tarehe 27 Ramadhani 1443 Hijria, ni Siku ya Kimataifa ya Quds. 

Imam Ruhullah Khomeini (M.A) Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran  aliitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds ili kuibakisha hai kadhia muhimu ya Palestina na kupawa Waislamu duniani kote fursa ya kutangaza mshikamano wao na Wapalestina sambamba na kukusanya nguvu kwa ajili ya kuikomboa Quds Tukufu kutoka kwenye makucha ya Wazayuni maghasibu.  

4053281

captcha