IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa

Palestina iko imara, ina azma ya kukomboa ardhi zake zinazokaliwa kwa mabavu na Israel

21:27 - April 29, 2022
Habari ID: 3475184
TEHRAN (IQNA)-Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema kuwa wananchi wa Palestina wamesimama kidete na wameazimia kuikomboa Palestina yote kutoka Bahari ya Mediterania hadi Mto Jordan.

Hujjatul Islam Walmuslimin Muhammad Javad Haj Ali Akbari ameongeza kuwa "Hii leo kuna maafikiano katika eneo la Palestina kuhusiana na kudumishwa  muqawama na mapambano dhidi ya Wazayuni maghasibu."

Akihutubia waumini walioshiriki Swala ya Ijumaa ya wiki hii iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Tehran, Sheikh Haj Ali Akbari amesema" Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Khamenei ameitaja Palestina kuwa ni madhlumu mwenye nguvu, kwani Palestina imedhulumika kweli na katika kipindi chote cha miaka 74 iliyopita ambapo kibla cha kwanza cha Waislamu na eneo hilo tukufu ambalo lilishuhudia miiraji ya Mtume (saw) linaendelea kukaliwa kwa mabavu na utawala usio na utambulisho na bandia ambao unaendelea kuvunjia heshima maeno matakatifu ya Waislamu. 

Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema, Palestina inadhulumiwa, na watu wake ambao wamekuwa wakiteseka kwa miongo saba, wakiuawa, kufukuzwa katika makazi yao, kuishi ukimbizini na kadhalika, wanaendela kustahamili mashaka ya aina mbalimbali; huku walimwengu na jumuiya zinazodai kutetea haki za binadamu zikiangalia kwa macho tu. Amesisitiza kuwa, eneo la Ukanda wa Ghaza sasa limegeuka na kuwa jela kubwa zaidi dunia. 

Haj Ali Akbari amesema: Watu madhulumu wa Palestina wamenyimwa haki ya maisha ya kawaida kwa miaka mingi na hadi sasa dunia haijaoneshwa hata asilimia mota tu ya masaibu na mateso yanayowapata watu wa Gaza. Amesema kuwa, Wapalestina wa Gaza wamesimama kidete kuwapinga wahalifu wakubwa zaidi ambao historia haijawahi kushuhudia mfano wao. Amesisitiza kuwa miongoni mwa maumivu ya Wapalestina ni kuona viongozi wanafiki na wasaliti wa baadhi ya nchi za Kiarabu wakifanya mapatano na utawala huo ghasibu.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran ameendelea kusema: Palestina ingali hai baada ya miaka 74 ya uvamizi, na imehifadhi utambulisho na asili yake dhidi ya utawala huo muovu.

Haj Ali Akbari amesema: "Palestina iko imara, imesimama kidete na imedhamiria kwa azma kubwa kukomboa ardhi yote iliyoghusubiwa kutoka Bahari ya Mediterania hadi Mto Jordan, na hii leo kuna maafikiano huko Palestina kwa ajili ya kudumisha muqawama na mapambano ya ukombozi."

Maandamano ya Siku ya Quds

Swala ya Ijuma ya leo mjini Tehran imefanyika baada ya maandamano makubwa ya mamilioni ya wananchi walioadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds. 

Leo Ijumaa tarehe 29 Aprili imesadifiana na tarehe 27 Ramadhani 1443 Hijria Qamaria, ni Siku ya Kimataifa ya Quds. 

Ijumaa ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ilitangazwa na mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Ruhullah Khomeini MA, kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Quds.

Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds nchini Iran yanafanyika kwa kushiriki wananchi katika maandamano baada ya kufanyika kwa miaka miwili kupitia misafara ya magari na kupitia intaneti kutokana na janga la corona.

Mbali na hapa nchini Iran, maandamano pia yamekuwa yakifanyika katika maeneo mbali mbali kote duniani na yataendelea wikiendi hii pia hasa katika nchi za Magharibi.

Wananchi wa Iran waliooshiriki katika maandamano ya leo wamesikika wakipiga nara za kuunga mkono taifa la Palestina linalodhulumiwa huku pia wakipiga nara za 'Mauti Kwa Israel', na 'Mauti kwa Marekani' sambamba na kulaani tawala za Kiarabu ambazo zimewasaliti Wapalestina kwa kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel.   

4053500

Habari zinazohusiana
captcha