IQNA

Jinai za Israel

Waziri wa Kizayuni aliyetaka bomu la nyuklia lidondoshwe Gaza sasa ataka Ramadhani 'ifutwe'

10:50 - March 02, 2024
Habari ID: 3478440
IQNA - Waziri wa utawala wa Kizayuni mwenye misimamo mikali ya chuki amesema mwezi mtukufu wa Ramadhani unapaswa 'kufutwa' ili kuepusha taharuki katika mji mtakatifu wa al-Quds (Jerusalem).

Waziri wa eti  turathi katika utawala haramu wa Israel, Amichai Eliyahu, aliiambia Redio ya Jeshi la Israel kwamba, "ule unaoitwa mwezi wa Ramadhani lazima ufutiliwe mbali, ili hofu yetu ya mwezi huu isiwepo."

Eliyahu ni mwanachama wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Otzma Yehudit, kinachoongozwa na waziri wa eti usalama wa taifa Itamar Ben Gvir.

Mwezi Novemba, Eliyahu alisema kudondosha "bomu la nyuklia" kwenye Ukanda wa Gaza ni "chaguo."

Hivi karibuni, uvujaji wa usalama wa Israel uliashiria hofu ya kuzuka kwa hali ya machafuko makubwa katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Mashariki ya al-Quds wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutokana na vita vya mauaji ya kimbari vya utawala wa Israel dhidi ya Ghaza na vikwazo ambavyo utawala wa Tel Aviv unakusudia kuliwekea Al- Msikiti wa Aqsa wakati wa Ramadhani.

Vyombo vya habari vya Israel vinasema kuwa utawala wa Marekani unaishinikiza Tel Aviv kufikia makubaliano na Hamas kuhusu kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza kabla ya Ramadhani, ambayo inaanza katika takriban siku 10 zijazo.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, alisema Alhamisi kwamba ni mapema kusema Tel Aviv imefikia makubaliano juu ya kubadilishana wafungwa na Hamas.

3487387

Habari zinazohusiana
captcha