IQNA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Amir- Abdollahian

Kura ya maoni iitishwe kuainisha mustakabali wa Palestina

10:51 - April 28, 2022
Habari ID: 3475179
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Utawala bandia wa Israel ni mkiukaji mkubwa wa haki za binadamu duniani huku akisisitiza kuwa kura ya maoni ni njia muafaka ya kuainisha mustakabali wa Palestina.

Tarehe 29 Aprili ambayo ni sawa na tarehe 9 mwezi Ordibehesht mwaka 1401 kwa kalenda ya Kiirani inasadifiana na tarehe 27 Ramadhani mwaka 1443 Hijria ambayo ni Siku ya Kimataifa ya Quds.

Imam Ruhullah Khomeini (M.A) Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran  aliitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds ili kuibakisha hai kadhia muhimu ya Palestina na kupawa Waislamu duniani kote fursa ya kutangaza mshikamano wao na Wapalestina sambamba na kukusanya nguvu kwa ajili ya kuikomboa Quds Tukufu kutoka kwenye makucha ya Wazayuni maghasibu. 

Hossein Amir- Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameandika katika makala iliyochapishwa katika gazeti la Al Quds al Arabi huko London kuwa: Kuhitimishwa uvamizi na kuitisha kura ya maoni itakayowashirikisha wakazi wote asili wa ardhi za Palestina na wakimbizi wote kwa ajili ya kuanisha mustakbali wao ni njia muafaka zaidi ya kuipatia ufumbuzi kadhia ya Palestina.  

Amir Abdollahian ameongeza kuwa: "Siku ya Kimataifa ya Quds ilianzishwa na Imam Khomeini ili kuunga mkono kadhia ya Palestina na kuanza awamu mpya ya mshikamano na wananchi wa Palestina.

Makala hiyo imeongeza kuwa, tangu kuasisiwa utawala haramu na bandia wa Israel mwaka 1948 hadi sasa ni moja ya sababu kuu za ukosefu wa amani na hali ya mchafukoge katika eneo la Magharibi mwa Asia. Amesema: Taifa lililodhulumika la Palestina limesimama imara na kuendeleza mapambano dhidi ya ukandamizaji na dhalma kubwa ya tawala huo bandia kwa uungaji mkono wa Waislamu na wapigania uhuru kote duniani. 

/678089

captcha