IQNA

Iran yataka Baraza la Salama la UN liache kunyamazia kimya jinai za Israel

19:43 - April 27, 2022
Habari ID: 3475175
TEHRAN (IQNA)- Balozi wa mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, kuna wajibu wa sheria za kimataifa kuulinda Msikiti wa al Aqsa ili kuzuia kutokea maafa yenye madhara makubwa.

Majid Takht-Ravanchi amesema hayo katika kikao cha jana Jumatatu cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichojadili matukio ya hivi karibuni ya Palestina na kulalalamikia vikali kutojali baraza hilo mateso wanayopatiwa Wapalestina na wanajeshi makatili wa Israel.

Amesema maadamu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litaendelea kudharau na kunyamazia kimya jinai za Israel, kamwe taifa la Palestina halitoweza kupata haki zake.

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, msimamo wa hivi sasa wa Baraza la Usalama unazidi kuupandisha kiburi utawala katili wa Israel na kuuchochea kuendeleza jinai zake dhidi ya wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.

Amesema, kuna ushahidi mkubwa na kamili wa jinai zinazofanywa na Israel dhidi ya wananchi wa Palestina. Jinai hizo zinakwenda kinyume kikamilifu na sheria za kimataifa na wajibu wa kulinda usalama na roho za raia. Jinai hizo zinakanyaga waziwazi hati ya Umoja wa Mataifa ambao kama utaonesha nia ya kweli unaweza kutumia sheria zake kuulazimisha utawala wa Kizayuni ukomeshe jinai zake hizo.

Aidha amegusia tuhuma zisizo na msingi wala mashiko za utawala wa Israel kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema kuwa, utawala wa Kizayuni unaeneza uongo kupitia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa shabaha ya kuficha jinai zake unazowafanyia wananchi madhlumu wa Palestina.

3478683

captcha