IQNA

Ukweli katika Qur'ani Tukufu kuhusu kutawassuli kupitia waja wema

17:27 - May 01, 2022
Habari ID: 3475193
TEHRAN (IQNA) - Kutawassuli maana yake ni mwanadamu afanye kiungo kati yake na Mwenyezi Mungu ili akidhiwe haja yake kwa sababu ya kiungo hicho

Kwa sababu hii, katika baadhi ya mila za Laylatul-Qadr, kumuomba Mwenyezi Mungu msamaha kunaambatana na kutawassuli.

Kutawassuli ni mojawapo ya dhana kuu ambayo inazingatiwa katika kuharakisha majibu ya maombi.

Kwa hiyo, moja ya ibada zinazozingatiwa katika Usiku wa Cheo yaani Laylatul Qadr ni kutawasali kupitia Ahlul-Bayt wa Mtume Muhammad SAW na kuomba msamaha. Lakini je, Qur'an inathibitisha dhana kama hiyo?

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ وَجَاهِدُوا فِي سَبِيلِهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

“Enyi mlioamini mcheni Mwenyezi Mungu na tafuteni njia ya kum- fikia. Na piganeni kwa ajili ya dini yake ili mpate kufaulu.” 

Al-Maida 35

Tawassuli ina maana ya kukaribia kitu kwa kupenda na kwa raghba. Kwa hiyo neno “tawassuli” lina maana pana na linajumuisha kazi yoyote na chochote kinachomleta mwanadamu karibu na Mungu.

Kama ambavyo Imamu Ali AS katika riwaya anasema: “Kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume, Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, neno la ikhlasi (La ilaha illa Allah), sala, zaka, funga ya Ramadhani, Hajj, kuwa na ukuruba na jamaa au sileh rahmi, kutoa sadaka waziwazi na kwa siri na amali zote njema"

Aya za Qur’ani zimetumika vyema kuwa njia ya kumweka mtu mwema mbele ya Mwenyezi Mungu na kumuomba Mwenyezi Mungu jambo kupitia kwa mtu mwema yake haikatazwi kwa namna yoyote ile na jambo hili halikinzani naTauhidi kidogo.

Katika ya 97 ta Surat Yusuf ya Qur'ani Tukufu tunasoma hivi:

قَالُوا يَا أَبَانَا اسْتَغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا إِنَّا كُنَّا خَاطِئِينَ

Wakasema: Ewe baba yetu! tuombee msamaha kwa dhambi zetu, hakika sisi tulikuwa wenye makosa.

Kwa mujibu wa aya hii, kuomba msamaha kupitia kwa mtu mwingine na hivyo si tu kwamba ombi hili halikinzani tauhidi, bali pia ni njia ya kupata neema ya Mwenyezi Mungu. Ni vipi Mtume Ya'qub alikubali ombi la watoto wake la istighfara na kuwapa jibu chanya? Hili linaonyesha kuwa kuomba kupitia waja wema au mawalii wa Mwenyezi Mungu kunajuzu na kupinga jambo hilo ni dalili ya kutoijua Qur'ani au ni chuki za uwongo zinazozuia kufikia ukweli wa mafundisho ya Qur'ani.

Nafasi ya mfano wa kiongozi wa kidini katika kuwaongoza wanadamu

Kusisitiza juu ya kutawassuli  ni muhimu kwa sababu muumini hutegemea chaguo la kiongozi wake na mwongozo anaopata kama  njia ya kumkaribia Mungu. Chaguo kama hilo, pamoja na kuwa mshikamano wa kihisia na njia ya msamaha na utimilifu wa dua, pia huweka kigezo cha mwongozo

Katika ya 64 Sura Nisaa tunasoma hivi:

وَمَا أَرْسَلْنَا مِنْ رَسُولٍ إِلَّا لِيُطَاعَ بِإِذْنِ اللَّهِ وَلَوْ أَنَّهُمْ إِذْ ظَلَمُوا أَنْفُسَهُمْ جَاءُوكَ فَاسْتَغْفَرُوا اللَّهَ وَاسْتَغْفَرَ لَهُمُ الرَّسُولُ لَوَجَدُوا اللَّهَ تَوَّابًا رَحِيمًا

"Na hatukumpeleka Mtume yeyote ila apate kutiiwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Na lau wangelikujia walipojidhulumu nafsi zao wakaomba msamaha kwa Mwenyeezi Mungu, na Mtume akawaombea msamaha, bila shaka wangemkuta Mwenyeezi Mungu, Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu."

Aya hii pia inasema kwa uwazi kwamba kwenda kwa Mtume SAW na kumweka kuwa muombezi mbele ya Mwenyezi Mungu na usuluhishi wake na uombezi wake ni wenye manufaa kwa wakosefu na kutapelekea kukubaliwa toba na rehema ya Mwenyezi Mungu. Bila shaka, uombezi huo unahitaji kuwepo kwa misingi na uwezo na utayarifu kwa wakosefu wenyewe.

captcha