IQNA

Qur'ani inasema Nini / 4

Ni Vipi Qur'ani Inatoa Muongozo?

17:21 - May 31, 2022
Habari ID: 3475320
TEHRAN (IQNA) - Vitabu vitakatifu katika dini mbali mbali mara nyingi huzingatiwa kama chanzo cha kuimarisha hali ya kiroho ya mtu na hii inaeleweka kama fikra ya mwongozo lakini Quran Tukufu ina misingi ya kipekee kuhusiana na nukta hii.

Mwongozo ambao Qur'ani natoa sio kwa eneo maalum la maisha ya mwanadamu. Hii ina maana kwamba Qur'ani imeangazia mahitaji yote ya mwanadamu.

Quran inatoa miongozo wa wakati wote; kutoka ukamilifu wa kiroho hadi masuala ya kijamii, utawala, haki, maadili, makabiliano na maadui, au kutatua uadui: “Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu.” (Surah Fussilat, aya ya 34).

Ikizungumzia familia Qur'ani Tukufu inasema inasema: “Na wale wanao sema: Mola wetu Mlezi! Tupe katika wake zetu na wenetu yaburudishayo macho, na utujaalie tuwe waongozi kwa wachamngu.” (Surah al-Furqan, aya ya 74) au “Na waozeni wajane miongoni mwenu na wema katika watumwa wenu na wajakazi wenu. Wakiwa mafakiri Mwenyezi Mungu atawatajirisha kwa fadhila yake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa Mwenye kujua.” (Sura an-Nur, aya ya 32).

Quran pia inaashiria suala la amani ya kiroho kama hitajio la kimsingi la mwanadamu, ikisema: “...Mwenyezi Mungu aliteremsha utulivu juu ya Mtume wake na juu ya Waumini...” (Sura Al-Fath, aya ya 26).

Maandiko haya matakatifu pia yanarejelea masuala mengine kama vile kushughulika na misukosuko ya ndani ambayo mtu hukabiliana nayo maishani, ikipendekeza watu watafute elimu na wafahamu maumbil. Aidha maandiko matakatifu  humshauri mwanadamu kusonga kwenye njia ya maarifa na kugundua ukweli, na kutoa mapendekezo ya  jinsi ya kuishi na wengine: “Wala usiwabeuwe watu, wala usitembee katika nchi kwa maringo. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila anaye jivuna na kujifakhirisha." (Surah Luqman, aya ya 18)

Hii inaonyesha kwamba Qur'ani inatoa mwongozo kwa sekta zote za maisha ya mtu na kwamba mafunzo yamo ndani ya Kitabu kwa ajili ya hatua yoyote na sehemu yoyote ya wanadamu.

Wale wanaodhani kuwa Qur'ani haizungumzii masuala yanayohusu maisha, siasa, uchumi na serikali wameghafilika na wanapuuza mambo. Sehemu kubwa ya Quran inarejelea nyanja hizi za kijamii za maisha.

Makala haya ni mukhtasari wa hotuba iliyotolewa na Ayatullah Seyyed Ali Khamenei katika mahafali ya Qur'ani Tukufu. Ayatullah Khamenei aliyezaliwa mwaka wa 1939 Miladia ni Marjaa Taqlid wa Kishia na ni Kiongozi Muadhamu Mapinduzi ya Kiislamu. Ameandika vitabu kadhaa kuhusu mafundisho ya Kiislamu.

Habari zinazohusiana
captcha