IQNA

22:39 - May 04, 2022
Habari ID: 3475206
TEHRAN (IQNA)- Qarii maarufu wa Misri, Sheikh Ahmed Ahmed Noaina amesoma Qur'ani Tukufu katika Msikiti wa Hagia Sophia huko Istanbul, Uturuki.

Kwa mujibu wa taarifa, katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Msikiti wa Hagia Sophia ulikuwa na shughuli mbali mbali zikiwemo vikao vya qiraa ya Qur’ani Tukufu, mihadhara na mawaidha.

Qarii mtajika wa Misri Sheikh Ahmed Ahmed Noaina wa ni miongoni mwa walioalikwa katika msikiti huo kwa ajili ya kuswalisha na kusoma Qur’ani Tukufu.

Maelfu ya waumini walishiriki katika Sala iliyosalishwa na Sheikh Noaina katika usiku wa Laylatul Qadr katika Msikiti wa Hagia Sophia.

Klipu hii hapa chini ni ya Sheikh Noaina akisoma aya za  Surah Az-Zukhruf

Sheikh Noaina  (Nuaina) alizaliwa mwaka 1954 katika mji wa Mutubas nchini Misri na alianza kujifunza Qur’ani Tukufu akiwa na umri wa miaka 4 na kuhifadhi Kitabu hicho Kitukufu akiwa na umri wa miaka minane.

Alijifunza mbinu ya qiraa ya Ustadh Mustafa Ismail huku akiendeleza masomo yake katika taalumu ya daktari wa watoto.

Noaina anatambuliwa kama mmoja kati ya wasomaji bora zaidi wa Qur’ani Misri na ulimwengu mzima katika zama hizi. Sheikh Daktari Nuaina ni qarii mtajika Misri na amepata umashuhuri kutokana na mbinu kumi tafauti anazotumia kusoma Qur'ani Tukufu.

Qarii huyu mashuhuri wa Misri amewahi kusoma katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani nchini Misri na nchi nyingi za Kiislamu. Mbali na kuwa msomaji wa Qur'ani pia amehifadhi kikamilifu kitabu hicho kitukufu. Taaluma nyingine ya Sheikh Nuaina ni daktari wa watoto.

4054529

Kishikizo: noaina ، qarii ، misri ، hagia sophia
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: