IQNA

Kuhifadhi Qur'ani

Wanafunzi 393 waliohifadhi Qur’ani wahitimu Istanbul

19:36 - June 03, 2022
Habari ID: 3475330
TEHRAN (IQNA)- Wanafunzi 393 waliohifadhi Qur’ani Tukufu wamehitimu katika mahafali iliyofanyika katika msikiti mmoja huko Istanbul, Uturuki.

Mahafali hiyo imefanyika katika Msikiti wa Arnavutkoy ambapo idadi kubwa ya wanafunzi waliohitimu na maafisa wa kidini Uturuki walishiriki.

Mufti Mkuu wa Istanbul Sheikh Safri Arpagu amesisitiza kuhusu umuhimu wa kuhifadhi Qur’ani na amesitiza nukta hiyo kwa kuashiria Hadithi ya Mtume SAW isemayo: “Mbora wenu ni Yule ambayo anaisoma Qur’ani na kuwafunza wengine.” Amesema waliohitimu katika mahafali hiyo wamepata baraka tele kutokana na kuwa wamehifadhi Qur’ani Tukufu.

Waislamu nchini Uturuki hujitokeza kwa wingi kusoma na kujhifuanza kuhifadhi Qur’ani Tukufu katika misikiti zaidi ya tisini elfu nchini humo.

Katika msimu wa majira ya joto mwaka huu, inatazamiwa kuwa vituo vya kuhifadhi Qur’ani vitazinduliwa katika mikoa yote nchini Uturuki.

Kwa mujibu wa takwimu, mwaka 2021, kuna wanafunzi 11,700 waliohifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu kote Uturuki.

4058934

captcha