Yeye pia ndiye Mwarabu wa kwanza aliyetayarisha tarjuma ya Qur’ani katika lugha ya Kifaransa.
Alizaliwa Oktoba 10, 1889, katika kijiji cha Laghouat nchini Algeria. Alienda katika shule ya Qur'ani na akaanza kuhifadhi Qur’ain huko akiwa bado mdogo.
Kisha akaenda shule ya Kifaransa huko Algeria. Ahmed alifanikiwa kupata digrii mbili za Uzamili au MA, moja mnamo 1913 na nyingine mnamo 1916.
Kisha akaanza kufundisha na pia kufanya kazi kama mshauri wa masuala ya sheria.
Ahmed pia aliandika vitabu na makala nyingi katika nyanja za dini, falsafa na historia na alitarjumi vitabu muhimu vya Kiislamu katika lugha ya Kifaransa.
Kazi yake kuu ilikuwa tarjumi ya Qur’ani Tukufu kwa Kifaransa kama Mwarabu wa kwanza kufanya hivyo.
Alikuwa na ujuzi wa utamaduni na mafundisho ya Kiislamu na alikuwa na nia ya kukuza mawazo ya Kiislamu. Pia alikuwa akiongea Kifaransa vizuri. Ndiyo maana alianza kutafsiri Qur’ani Tukufu kwa Kifaransa.
Alianza kazi hiyomwaka wa 1926 na kuichapisha mwaka wa 1931 chini ya jina la "Le Coran".
Tangu kuchapishwa kwake, tarjumi yake ya Qur’ani imekuwa marejeo makubwa kwa wasomi na watafiti wa Kiislamu.
Lengo lake kuu la katika kazi hiyo yenye thamani lilikuwa ni kukuza Uislamu, kwani aliona ni muhimu kutumia lugha za kigeni kueneza Uislamu na mafundisho ya Mtukufu Mtume (SAW).
Kazi yake ilikuwa na nafasi kubwa katika kuutambulisha Uislamu kwa Wazungu na ulimwengu unaozungumza Kifaransa.
Kutokana na juhudi zake, maelfu nchini Ufaransa na nchi nyingine za Ulaya walisilimu. Ahmed al-Aimash alifariki mwaka 1959 akiwa na umri wa miaka 70.
4234837