TEHRAN (IQNA)- TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini Algeria imetangaza kuwa fainali ya Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani nchini humo itafanyika kunazia tarehe 15 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Duru ya mchujo ilifanyika katika mikoa mbali mbali nchini humo ambapo washindi wameingia fainali
Afisa wa wizara hiyo Masoud Miad amesema kila kati ya mikoa yote 58 nchini humo itakuwa na wawakilishi wawili katika fainali za kitaifa.
Aidha amesema washindi wa mashindano hayo wataenziwa na kutunukiwa zawadi katika sherehe zitakazofanyika katika usiku wa 27 wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Algeria kila mwaka pia huwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani lakini mwaka huu yamefanyika Mwezi wa Rajab.