IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran ni Mfano kwa Nchi nyingine

16:27 - June 15, 2022
Habari ID: 3475380
TEHRAN (IQNA) - Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndiyo mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yanayoaminika na yenye itibari zaidi duniani, afisa mmoja alisema.

Hamid Majidimehr, Mkuu wa Kituo cha Masuala ya Qur'ani cha Shirika la Iran la Wakfu na Misaada, ameongeza kuwa, katika kipindi cha miaka miwili iliyopita nchi nyingi zilisimamisha na kuahirisha mashindano yao ya Qur'ani kwa sababu ya janga la corona, lakini Iran iliandaa mashindano yake kama ilivyokuwa imepangwa kwa utaratibu ambao ulichukuliwa kama mfano na baadhi ya nchi.

Malaysia ambayo ina uzoefu wa kuandaa mashindano 62 ya kimataifa ya Qur'ani ni kati ya nchi ziliozahirisha mashindano ya Qur'ani, alisema.

Afisa huyo aliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Qom kuhusu mashindano ya 45 ya kitaifa ya Qur'ani ya Iran.

Amesema katika mashindano ya Qur'ani ya nchi nyingine, mashindano yenyewe ndiyo jambo kuu lakini nchini Iran, lililo muhimu zaidi ni kuandaa mazingira ya kujikurubisha zaidi kwenye Kitabu Kitukufu na kuelekea kwenye kutafakari na kutenda amali kwa nia safi.

Majidimehr pia aliashiria kiwango cha juu cha jopo la majaji katika mashindano ya Qur'ani ya Iran, akisema wataalamu bora na waliobobea zaidi wa Qur'ani wanahudumu katika jopo la majaji.

Amebainisha kuwa kuna baadhi ya wataalamu 5,000 wa Qur'ani nchini Iran ambao wana vyeti vya juu vya katika mashindano ya Qur'ani.

Wataalamu wa kigeni wa Qur'ani wanaokuja Iran kuhudumu katika jopo la majaji  baadaye huiga kanuni za mashindano ya Qur'ani ya Iran.

Kwingineko katika matamshi yake,, Majidimehr amesema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ndiye muungaji mkono mkubwa wa wanaharakati wa Qur'ani nchini Iran na ulimwengu wa Kiislamu.

Shirika la Wakfu na Misaada la Iran kila mwaka huandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kwa kushirikisha wanaharakati wa Qur'ani kutoka nchi mbalimbali.

Washindani 62 kutoka nchi 29 walishiriki fainali ya Mashindano ya 36 ya Kimataifa ya Iran yaliyofanyika mwezi Machi.

84788256

captcha