IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran yanaongoza kwa idadi ya washiriki duniani

19:06 - November 22, 2024
Habari ID: 3479791
IQNA - Afisa mmoja wa Iran amesema mashindano ya kila mwaka ya kimataifa ya Qur'ani  ya Iran yana idadi kubwa zaidi ya washiriki kati ya matukio ya kimataifa ya Qur'ani katika ulimwengu wa Kiislamu.

Mkuu wa Kituo cha Masuala ya Qur'ani cha Jumuiya ya Awqaf na Misaada Hamid Majidimehr amesema hayo katika kikao na Ayatullah Ali Reza A'rafi, Mkurugenzi wa Vyuo Vikuu vya  Kiislamu (Hauza) nchini Iran.

Amebainisha kuwa wasomaji na wahifadhi Qur'ani kutoka nchi 110 walishiriki katika duru ya 40 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran, yaliyofanyika Tehran tarehe 15-19 Februari 2024.

Amesema hii dalili kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaungwa mkono katika maeneo yote ya dunia.

Afisa huyo pia alibainisha kuwa wakati wa janga la coronavirus, nchi 27 za Kiislamu zilifuta mashindano yao ya kimataifa ya Qur'ani lakini Iran ilifanya mashindano yake, katika ngazi ya kitaifa na kimataifa, na nchi zingine zikaanza kuiga mfano huo.

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huandaliwa kila mwaka na Jumuiya ya Masuala ya Wakfu na Misaada Iran.

Mashindano hayo hulenga kukuza utamaduni na maadili ya Qur'ani miongoni mwa Waislamu na kuonyesha vipaji vya wasomaji na wahifadhi Qur'ani.

Habari zinazohusiana
captcha