IQNA

Mchakato wa Mashindano ya Qur'ani ya Kitaifa ya Iran waendelea

16:27 - November 05, 2024
Habari ID: 3479707
IQNA - Mchakato wa kutathmini washiriki wa hatua ya awali ya Mashindano ya 47 ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran umeanza leo  Jumanne, Novemba 5


Wajumbe wa jopo la majaji wamekusanyika katika makao makuu ya Shirika la Wakfu na Masuala ya Hisani mjini Tehran kwa ajili ya tathmini katika sehemu mbili za wanaume na wanawake.
Jopo hilo limetazama klipu zilizorekodiwa za washiriki ambao wamefika hatua ya kitaifa.
Watakaopata alama bora watafuzu kwa hatua ya mwisho ya mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika Desemba katika mji wa kaskazini-magharibi wa Tabriz.
Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kila mwaka huandaliwa na Shirika la Wakfu na Masuala ya Hisani kwa kushirikisha wanaharakati wakuu wa Qur'ani kutoka kote nchini.
Mashindano hayo yanalenga kugundua vipaji vya Qur'ani na kukuza shughuli za Qur'ani katika jamii.
Washindi wakuu wa mashindano hayo wataiwakilisha Iran katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kote duniani.
Mashindano ya mwaka huu yanafanyika katika chini ya kauli mbiu ya "Kuwakumbuka Mashahidi wa Huduma",  yaani Rais wa zamani Ebrahim Raisi na wenzake waliokufa shahidi katika ajali ya helikopta mwezi Mei.

3490565

Habari zinazohusiana
captcha