IQNA

Mashindano ya Pili ya Usomaji Qur'ani wa kuiga nchini Iran

21:25 - February 18, 2025
Habari ID: 3480237
IQNA – Toleo la pili la Tamasha la Usomaji Qur'ani wa Kuiga sauti za maqari mashuhurilinatarajiwa kufanyika katika mji wa Qazvin, Iran, kuanzia Februari 22 hadi 25, likiwakutanisha maqari  50 vijana kutoka sehemu mbalimbali za nchi.

Akizungumza na IQNA, Hujjatul Islam Seyed Mostafa Majidi, Mkurugenzi Mkuu wa Mambo ya Wakfu na Hisani katika Mkoa wa Qazvin, amesema kwamba mashindano hayo yatafanyika katika makundi matatu ya umri: miaka 9-13, 13-16, na 16-20.

Kwa mujibu wa Majidi, zaidi ya vijana 3,000 wenye shauku ya Qur’ani walituma usomaji wao mtandaoni baada ya kutangazwa kwa tamasha hilo. Alieleza kuwa:, “Baada ya mchujo wa awamu tatu, majaji walichagua washiriki 50 wa fainali, ambao watakusanyika Qazvin kwa mashindano.”

Ratiba ya mashindano inaonyesha kuwa mashindano yataanza jioni ya Februari 22 na kuendelea hadi Februari 24, huku fainali ikifanyika Februari 24 na hafla ya kufunga ikifanyika Februari 25.

Majidi alieleza kuwa, mbali na tukio kuu, kutakuwa na mikusanyiko ya Qur’ani inayohusisha Qari wa kimataifa na wa ndani katika mkoa mzima wa Qazvin. “Tumepanga vikao 22 vya Qur’ani ili kuboresha mazingira ya tamasha, pamoja na maonyesho ya bidhaa za Qur’ani na utamaduni katika eneo la Imamzadeh Hossein.”

Tamasha la mwaka huu linajengwa juu ya mafanikio ya tukio la kwanza, ambalo lilianzisha dhana ya usomaji wa kuiga – ambapo washiriki huiga mitindo ya wasomaji mashuhuri wa Qur’ani – kwa hadhira pana zaidi.

Tamasha la mwaka jana lilifanyika katika Imamzadeh Saleh, Tehran, mnamo Mei.

3491905

Habari zinazohusiana
captcha