IQNA

Kuhifadhi Qur'ani

Maelfu ya wavulana, wasichana wahitimu kuhifadhi Qur'ani Uturuki

13:11 - June 29, 2022
Habari ID: 3475440
TEHRAN (IQNA)- Zaidi ya wanafunzi 8,000 wa Uturuki wamehitimu katika somo la kuhifadhi Qur'ani Tukufu katika kozi ambayo imedumu mwaka moja

Kwa mujibu wa taarifa, wavulana na wasichana 8,695 wa Uturuki wamefanikiwa kuhifadhi Qur'ani kikamilifu katika mwaka wa masomo wa 2021-22.

Wamepokea vyeti vya kuhifadhi Qur'ani kutoka Idara ya Masuala ya Kidini ya Uturuki (Diyanet) baada ya kutimiza vigezo vyote. Mwaka jana wanafunzi wengine 73,000 walishiriki katika kozi za kuhifdhi Qur'ani kote Uturuki katika mwaka uliopita.

Kwa mujibu wa Diyanet, jumla ya watu  zaidi ya laki mbili Uturuki wana vyeti vya kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

Kuna misikiti takribani 90,000 Uturuki na kila mwaka huandaa masomo maalumu ya kuhifadhi Qur'ani, Tafsiri na masomo mengine ya Kiislamu.

4067296

captcha