IQNA

Sala ya Ijumaa Tehran

Eneo la Asia Magharibi liko mikononi mwa Waislamu na si Marekani

19:43 - July 01, 2022
Habari ID: 3475447
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema eneo la Asia Magharibi halidhibitiwi tena Marekani, na kwamba hivi sasa lipo katika mikono ya mataifa ya Waislamu.

Hujjatul-Islam Walmuslimin Sayyid Muhammad Hassan Abu Turabi-Fard amesema hayo katika hotuba za Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa Tehran na kuongeza kuwa, "Miito ya baadhi ya watu ya kutaka kuundwa muungano wa kijeshi wa NATO katika eneo la Kusini Magharibi mwa Asia inatokana na ukweli kwamba, wanashuhudia kuimarika nguvu ya Umma wa Kiislamu."

Imamu huyo wa muda wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran ameeleza kuwa, muungano huo wa kijeshi wa eti NATO ya mamluki wa Marekani hautakuwa na athari zozote mkabala wa harakati zenye mamlaka na nguvu katika eneo.

Hujjatul-Islam Walmuslimin Abu Turabi-Fard amesisitiza kuwa: Eneo la Mashariki ya Kati haipo tena katika udhibiti wa Marekani, lakini lipo mikononi mwa Waislamu wa eneo hili.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran ameashiria umuhimu wa kufungamana na uadilifu katika maisha ya kila siku ya mwandamu kama wajibu wa kiroho na kubainisha kuwa: Waislamu wanapaswa kueneza haki ili washuhudie ustawi mkubwa katika ulimwengu wa Kiislamu.

4067799

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :