IQNA

Bendera ya Ghadir yapandishwa katika Haram ya Imam Ali AS

23:39 - July 15, 2022
Habari ID: 3475507
TEHRAN (IQNA)- Kwa mnasaba wa kuwadi siku kuu ya Idul Ghadir, kumefanyika sherehe ya kupandisha bendera ya Ghadir katika Haram ya Imam Ali (AS).

Katika bendera hiyo kumeandikwa Mtu ambaye mimi ninamsimamia mambo yake, (yaani ambaye mimi ni kiongozi wake) basi na huyu Ali naye anamsimamia mambo yake.”

Maafisa wa Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Imam Ali AS mjini Najaf, Iraq pamoja na wawakilishi wa wanazuoni, wanasiasa, maafisa wa usalama, wasomi na wafanyaziara walishiriki katika hafla hiyo.

Kumepangwa hafla kadhaa katika haram hiyo takatifu kwa mnasabwa wa Idul Ghadir ikiwa ni pamoja na mashindano ya kuhifadhi Qur’ani na warsha kadhaa.

Inafaa kuashiria hapa kuwa, 18 Mfunguo Tatu Dhulhija  miaka1433 iliyopita Mtume Muhammad (SAW) akiwa katika safari yake ya mwisho ya Hija, kwa amri ya Mwenyezi Mungu alimtangaza Imam Ali bin Abi Twalib AS kuwa kiongozi wa Waislamu wote baada yake. Hatua hiyo ya Mtume Mtukufu ilifanyika katika eneo linalojulikana kwa jina la Ghadir Khum katika makutano ya njia ya Makka na Madina. Siku hiyo Mtume SAW alitoa hotuba mbele ya hadhara kubwa ya Waislamu kisha akashika mkono wa Ali bin Abi Twalib na kusema: "Kila mtu ambaye mimi ni kiongozi wake basi huyu Ali pia ni kiongozi wake. Mwenyezi Mungu ampende atakayempenda, na amfanyie uadui atakayemfanyia uadui."

Mtume SAW pia aliwausia Waislamu kushikamana na Qur'ani na Ahlubaiti wake na akasema viwili hivyo havitatengana hadi vitakapomkuta yeye katika Hodhi ya Kauthar, Siku ya Kiyama.

Kwa mnasaba wa siku hii ya Idul Ghadir hufanyika sherehe na hafla katika nchi mbali mbali duniani. Mwaka huu siku kuu ya Ghadir inasadifiana na Julai 18.

4070837

captcha