Idara hiyo imetangaza kwamba maandalizi yote muhimu yamefanywa ili kusherehekea tukio hilo la furaha.
Ahmed al-Qureishi, idaya hiyo, alisema mipango na shughuli mbalimbali zimepangwa kuandaliwa katika ngazi ya ndani, kitaifa na kimataifa ili kusherehekea Eid al Ghadir.
Ni pamoja na sherehe mbalimbali za kitamaduni, kidini na kijamii, alisema.
Alibainisha kuwa Idara ya Mfawidhi wa Haram (kaburi) takatifu ya Imam Ali (AS).Astan itafanya sherehe nchini Iraq pamoja na nchi nyingine 12.
Kwa mujibu wa Haidar Rahim, afisa mwingine wa idara hiyo, bendera ya kaburi takatifu la Imam Ali (AS) itapandishwa katika maeneo 40 nchini Iraq na nchi nyinginezo zikiwemo katika majimbo 12 ya Ulaya.
Amesema, Haram tukufu ya Imam Ali (AS) itakuwa na programu mbalimbali zikiwemo duru za Qur'ani, tamasha za fasihi, vikao vya wanazuoni na shughuli za sanaa katika wiki ya kuelekea Eid al-Ghadir.
Mapema mwaka huu, bunge la Iraq lilitangaza sikukuu ya Eid al-Ghadir kuwa siku ya mapumziko katika nchi hiyo ya Kiarabu.
Tukio la Ghadir, au Eid al-Ghadir, linaloadhimishwa Jumanne, Juni 25 mwaka huu, huadhimishwa na Waislamu wa Shia duniani kote kila mwaka. Ni miongoni mwa sikukuu muhimu za Waislamu wa madhehebu ya Shia na hufanyika siku ya 18 ya Dhul Hijjah katika kalenda ya Hijria Qamaria.
Ilikuwa ni siku ambayo kwa mujibu wa riwaya za kuaminika, Mtukufu Muhammad (SAW) alimteua Ali ibn Abi Talib (AS) kama khalifa wake na Imam baada yake mwenyewe kwa kufuata amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
4222437