IQNA

Sherehe katika Haram Takatifu ya Imam Ali AS mkesha wa Siku Kuu ya Ghadir

19:58 - July 28, 2021
Habari ID: 3474135
TEHRAN (IQNA)- Sherehe imefanyika katika Haram Takatifu ya Imam Ali AS mjini Najaf, Iraq ambapo wanaohudumu katika eneo hilo takatifu wametangaza utiifu wao kwa Imam Ali AS.

Sherehe hiyo ilianza kwa qiraa ya aya za Qur'ani Tukufu. Waislamu wa madhehebu ya Shia kote duniani wameanza kuaadhimisha sikukuu ya Ghadir ambayo ni kati ya siku muhimu zaidi katika kalenda ya historia ya Uislamu.

18 Dhulhija takribani 1431 iliyopita Mtume Muhammad SAW akiwa katika safari yake ya mwisho ya Hija, kwa amri ya Mwenyezi Mungu alimtangaza Imam Ali bin Abi Twalib AS kuwa kiongozi wa Waislamu wote baada yake.
Hatua hiyo ya Mtume Mtukufu ilifanyika katika eneo linalojulikana kwa jina la Ghadir Khum katika makutano ya njia ya Makka na Madina.  Siku hii huadhimishwa kama  Siku Kuu ya Ghadir.

 

 

3987033

 

captcha