IQNA

Qur'ani Tukufu Inasemaje /18

Aya ya Ukhalifa katika Qur'ani Tukufu; Kuchagua Mrithi wa Mtume Muhammad (SAW)

11:43 - July 16, 2022
Habari ID: 3475508
TEHRAN (IQNA) – Baada ya kuteremshwa aya inayozungumzia kuteuliwa kwa Harun kama naibu wa Musa, Mtume Muhammad (SAW) alimteua mrithi wa ukhalifa wake na hadithi hii imetajwa na wanazuoni na wanahistoria wengi wa Kiislamu kutoka asili tofauti.

Moja ya masuala muhimu kuhusu serikali ya kidini ni kuteua mtawala. Katika serikali ambazo zilianzishwa na manabii, kama vile Suleiman, ni nabii aliyeongoza serikali. Lakini swali ni je, ni nani atakayechukua nafasi yake baada ya kifo chake?

Nafasi hii, ambayo inajulikana kama khalifa, ilipata maana kwa Mtume Muhammad (SAW) wakati alipoanzisha serikali huko Madina. Katika Hadith sahihi, hata hivyo, Mtume (SAW) alimteua mrithi wake na riwaya hii  imetajwa na takriban madhehebu zote za ya Kiislamu. Hadith hii inahusiana na moja ya aya maarufu za Qur'ani Tukufu kuhusu Nabii Musa AS ambayo wakati mwingine inajulikana kama "aya ya ukhalifa".

“Tulimuahidi Musa masiku thalathini na tukayatimiza kwa kumi; ikatimia miadi ya Mola wake Mlezi masiku arubaini. Na Musa akamwambia nduguye Haarun: Shika mahala pangu kwa watu wangu na utengeneze wala usifuate njia ya mafisadi." (Surah Al-A'raf, aya ya 142)

Akiashiria aya hii, Mtume Muhammad (SAW) alimhutubu Imam Ali (AS) na kusema: “Wewe ni kama Harun alivyokuwa kwa Musa, isipokuwa hakuna Mtume baada yangu.”

Mtume Muhammad (SAW) aliashiria mtazamoa huu  mara kadhaa lakini mfano maarufu zaidi ulikuja kabla ya msafara wa Tabuk katika mwaka wa 9 Hijria; Mtume (SAW) alimteua Imam Ali (AS) kama mrithi wake huko Madina kabla ya kuanza safari ya kwenda Tabuk. Nafasi ya Imam Ali (AS) ilikuwa na umuhimu mkubwa kutokana na umbali wa Tabuk na pia wasiwasi wa kiusalama ambao ulitishia Madina. Zaidi ya uteuzi huu, jinsi Mtume (SAW) alivyomuelezea Imam Ali (AS) inaonyesha taratibu maalumu ambayo haijafuatwa kuhusiana na masahaba wengine wowote wa Mtume Muhammad (SAW).

Hadithi hii pamoja na ile ya Ghadir Khumm inaashiria Wilaya ya Imam Ali (AS) na ni muhimu kwa sababu kwanza, imetajwa mara kwa mara na Mtume Muhammad (SAW) kama vile katika vita vya Tabuk, na pili, inampa Imam Ali (AS) hadhi ya Mtume isipokuwa hakuwa na utume. Na Mtume Muhammad (SAW) hakuwahi kumuondoa Imam Ali kwenye nafasi hii.

Mwanacuoni maarufu wa Kiislamu Ibn Asakir (1106-1176 Miladia) aliitaja hadithi hii katika kitabu chake "Historia ya Damascus" kupitia vyanzo 144 huku mwanachuoni mwingine wa Kiislamu aitwaye Imam An-Nasai ameitaja hadithi hiyo na kuifungamanisha na vyanzo au marejeo 33.

3479650

Habari zinazohusiana
captcha