IQNA

18:41 - July 29, 2021
News ID: 3474139
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa kumpenda na kumfuata wasii wa Mtume Muhammad (SAW), Imam Ali bin Abi Twalib (AS) ndiyo njia ya uokovu na kujikwamua katika makucha ya mabeberu.

Akizungumza leo Sayyid Abdul Malik Badreddin al Houthi amesema madola ya kibeberu yakiogozwa na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel yanafanya mikakati ya kuudhibiti Umma wa Kiislamu na kuongeza kuwa, mbinu inayotumiwa na mabeberu hao kwa ajili ya kufikia malengo yao ni kuzusha machafuko, migawanyiko na migogoro katika Umma. 

Al Houthi amesema kuwapenda na kuwafuata Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad (SAW) ni jambo la dharura katika kuupa kinga Umma wa Kiislamu mbele ya njama za fitina za maadui na kuongeza kuwa: Hatupasi kuyaruhusu madola ajinabi kuudhibiti Umma wa Kiislamu.

Katibu Mkuu wa Mapinduzi ya Watu wa Yemen amesema lengo la kumpenda na kumfuata Imam  Ali bin Abi Twalib (SAW) ni kudumisha njia ya uokofu ya Mtume Muhammad (SAW), kusimamisha dini barabara na kujiepusha na upotoshaji. 

Wayemen wamejitokeza kwa maelefu kuadhimisha siku kuu ya Ghadir katika mji mkuu Sanaa na pia katika mikoa ya Amran, Jowf, Maarib, Hajja, Taiz, Hudaida, Al Bayda, Al Mahwit, Ibb, Dhamar, Dhale na Raymah

Siku ya leo tarehe 18 Mfunguo Tatu Dhulhija kwa mujibu wa mapokezi ya wanahisoria na hadithi inakumbusha tukio la Ghadir Khum wakati wa Hija ya Mwisho wa Mtume Muhammad (SAW) maarufu kama Hajjatul Wida'.

Siku hiyo Mtume Muhammad (SAW) alitoa hotuba mbele ya hadhara kubwa ya maelfu ya Waislamu kisha akashika mkono wa Ali bin Abi Twalib na kusema: "Kila mtu ambaye mimi ni kiongozi wake basi huyu Ali pia ni kiongozi wake. Mwenyezi Mungu ampende atakayempenda, na amfanyie uadui atakayemfanyia uadui." Mtume (saw) pia aliwausia Waislamu kushikamana na Qur'ani na Ahlubaiti wake na akasema viwili hivyo havitatengana hadi vitakapomkuta yeye katika Hodhi ya Kauthar, Siku ya Kiyama.

3987230

Tags: yemen ، ansarullah ، ghadir
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: