IQNA

Njama za Wazayuni

Maulamaa wa Yemen walaani watawala wa Saudia walioruhusu Yahudi aingie Makka

22:35 - July 23, 2022
Habari ID: 3475528
TEHRAN (IQNA)- Chama cha wasomi wa Kiislamu Yemen kimesema watawala wa Saudi Arabia hawastahili kusimamia maeneo matakatifu zaidi ya Kiislamu ya Makka na Madina baada Yahudi Muisraeli kuachwa kuingia katika maeneo hayo.

Katika taarifa, wanazuoni hao wa Yemen wamelaani vikali kuvunjiwa heshima mji mtakatifu wa Makka na mwandishi habari Yahudi Muisraeli.

Gil Tamary ambayo ni Yahudi mwandishi habari wa kituo cha televisheni cha Channel 13 cha utawala wa Kizayuni wa Israel Jumatatu alituma video katika ukurasa wake wa  Twitter akiwa ameingia katika mji mtakatifu wa Makka  eneo ambalo ni marufuku kwa wasio Waislamu kuingia. Hatua hiyo imewakasirisha Waislamu ulimwenguni kote.bb

Chama cha wasomi wa Yemen kilisema katika taarifa kwamba kilitazama kwa uchungu mkubwa na kulaani taarifa kuwa mwandishi habari Yahudi Mzayuni  alifika katika maeneo matakatifu ya Makka na Madina wakati wa msimu wa Hija mwaka huu.

Wanazuoni hao wa Yemen wanasema kitendo hicho cha dharau na kuvunjia heshima Uislamu kimenyamaziwa kimya na wanazuoni wa  Kiislamu Saudia na kusema wanapaswa kuvunja kimya chao na kulaani kitendo hicho kiovu ambacho kimetekelezwa kwa idhini ya watawala wa Saudia. Taarifa hiyo imesema watawalawa wa Saudia wamevunjia heshima maeneo matakatifu ya Makka na Madina kwa kuwaruhusu makuhani wa Kiyahudu na vyombo vyao ya habari kuingia katika maenei matakatifu.

Jumuiya hiyo ya Maulamaa imesema ukimya, kutokujali na ukosefu wa msimamo mkali dhidi ya kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu ni jambo ambalo  linaloweza kuhimiza kukaririwa matukio kama haya.

Jumuiya hiyo ilitaka wasomi wa ulimwengu wa Kiislamu kukemea harakati za serikali ya Saudia ambayo iko mbioni kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Pia ilihimiza mataifa ya Waislamu kufanya mikutano ya maandamano dhidi ya sera za ufalme wa Saudia.

Ofisi ya kisiasa ya Yemen's Ansarullah Maarufu harakati pia ililaani uhalifu uliofanywa na watawala wa Saudia ambao wameruhusu uwepo wa Wayahudi katika eneo takatifu la Kiislamu wakati waliwazuia mamilioni ya Waislamu kuhudhuria ibada ya Hija mwaka huu.

4072582

captcha